Tukusaidie vipi?
Majibu ya maswali ya kawaida, na mtu wa kumwandikia yasipotosha.
Tuandikie
Tuambie namba ya simu au barua pepe ya akaunti yako na kilichotokea. Tunajibu kwa Kiswahili, Kiingereza au Kifaransa.
support@talatala.appPicha, krediti na malipo
Nimelipa lakini krediti hazijafika
Pesa ya simu inaweza kuchukua dakika chache kuthibitishwa. Krediti zikikosekana baada ya hapo, mwandikie support@talatala.app ukitaja namba uliyolipia na saa ya malipo.
Picha imeshindikana au haikukamilika
Mwandikie support@talatala.app ukitaja mtindo uliochagua na takriban saa. Tunachunguza kila picha iliyoshindikana.
Picha haifanani nami
Tumia selfie zenye mwanga mzuri, uso ukitazama kamera na bila kitu kinachoufunika. Selfie tatu tofauti zinasaidia zaidi kuliko moja.
Naweza kutengeneza picha za mtu mwingine?
Ikiwa tu amekuambia wazi kuwa unaweza kutumia picha zake. Kumweka mtu bila ridhaa yake ni kuvunja masharti ya matumizi na akaunti yako itafungwa.
Nafutaje akaunti au picha zangu?
Mwandikie support@talatala.app kutoka kwa barua pepe au namba ya simu ya akaunti yako na utuambie cha kufuta.